
Hautaniweza wee!
female voice, swahili taarab with flair, contemporary taarab, groovy bass, kenyan coastal style and accent
July 21st, 2024suno
Lyrics
[Hype Shout Out]
Monkey Jams!
[Hype Taarab Intro]
(Halo - Halooooh!
Ulinifanyia dharau na wale vibaraka sasa nyumba hiiiih! uione paah!)
[Verse]
Hauniwezi wee sura ya pweza
Tangu nikuache sijakupeza
Wafate wale waliokupoteza
Maana mie nakubeza
[Verse 2]
Moyo wangu sio chenza
Sitaki zako bembeleza
Sina muda wa kupoteza
Sina hali ya kucheza
[Chorus]
Uliowamumunya sasa meza
Ladha ya chumvi imekoleza
La maisha ninasongeza
Nishampata anayenipenza
Uliowamumunya sasa meza
Ladha ya chumvi imekoleza
La maisha ninasongeza
Nishampata anayenipenza
(Ulidhani muwa wako ndio wa pekee... eeh?
Kuna wengine wenye ekari baaaah-buuuuh!)
[Verse 3]
Mapenzi yangu kwako uliyaisha
Michezo ya sesere na Aisha
Nikijaribu kutafuta maisha
Vituko vya kwako nimekwisha
[Bridge]
Usinifuate usinirudie
Hakuna chako cha zamani
Samahani zako siniambie
Mie hapa nina wangu hanih!
[Chorus]
Uliowamumunya sasa meza
Ladha ya chumvi imekoleza
La maisha ninasongeza
Nishampata anayenipenza
Uliowamumunya sasa meza
Ladha ya chumvi imekoleza
La maisha ninasongeza
Nishampata anayenipenza
(ulichelewa huko kwa bikizee, basi mwanamwali akafuata asali....
ukiona vyaeleaaah! vimeundwaaaah!)
[Outro][Repeat]
Ninaye wangu seremala
Hodari sana kupiga randa
Fundi mwenye ujuzi na ala
Kwanza ezeka chako kibanda
(Monkey Jams!)
[Applause]
Recommended

A World To Dream Of
alternative rock. britpop. indie. soul. psychedelic.

失業
Heavy Female Voices, mutation funk, Horror Vibes, Electric guitar intro, guitar diff, rap, j-pop,ukrainian electro

“Never the Same”
dark, rock

魔法の冒険
enchanting pop lively

Without my baby I'm broken
Soul Blue, blues, blues

Kojukarin Kesäpäivä
male vocalist,folk,contemporary folk,regional music,poetic,nature,melancholic

Filhos do Trovão
pop anthemic

Лера Карамелькина
романтичная поп летняя
The Final Siren
instrumental,electronic,post-industrial,industrial & noise,drone,dark ambient,bassline,synthesizer

Children of the Dark
hardstyle, violin, trance, bass, synth

run in the rain
pop, jazz

Rekursion
electronic edm

Mary's Dream
raw rock electric

Practice
Dakar Future Bass

Танцы в Полуночи
энергичная танцевальная поп-музыка женский вокал